Jumapili 15 Juni 2025 - 21:14
Iran kwa jibu la kushtua, ilipiga anga ya Israel na kuonesha uwezo wake wa kiutawala

Hawza/ Mkuu wa Kituo cha Harakati za Kiutamaduni na Kijamii cha Tabyan cha Afghanistan, kwa kutoa tamko kuhusiana na jibu la kushtua na la wazi lililotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika operesheni ya “Ahadi ya Kweli 3”, alisisitiza: Kuanzia usiku uliopita hadi alfajiri ya leo, kilele cha utukufu, uwezo na busara ya Wairani kimeoneshwa kuliko wakati wowote ule.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini kamili ya tamko la Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Isa Husayni Mazari, Mkuu wa Kituo cha Harakati za Kiutamaduni na Kijamii cha Tabyan Afghanistan, kuhusu jibu la kushtua la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa jinai za utawala wa Kizayuni, ni kama ifuatavyo:

Bismillāhi Rahmāni Rahīm

Katika historia yote, ni nadra kupatikana usiku kama wa jana, tarehe 23 Jawza / Khurdād 1404, ambao tumeshuhudia kazi ya kipekee namna hiyo kutoka kwa taifa na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Usiku ambao hadi alfajiri ya leo, kilele cha utukufu, uwezo na hekima ya Wairani vimeoneshwa katika uwanja wa kihistoria na wenye hatima, kuliko wakati wowote ule.

Katika hali ambapo uwanja mzima wa ukafiri na uzushi, pamoja na vibaraka wao, wamesimama katika safu moja pamoja na utawala batili wa Kizayuni, unao uwa watoto — na wataendelea kusimama nao endapo utawala huu utaendelea kuwepo — Iran imepigana kwa nguvu katika pande mbili kwa wakati mmoja, na ikatoka katika mtihani huu wa kimungu ikiwa imetukuka na imara.

Pamoja na kuwa katika saa za mwanzo adui alifanya shambulio la ghafla na kuwaua kishahidi baadhi ya wapendwa zaidi na muhimu wa kijeshi wa Iran — wapendwa ambao walikuwa na mpango wa utekelezaji na taarifa za malengo ya adui mikononi mwao — lakini jibu la Iran lilikuwa kama radi kali iliyolipua anga ya utawala wa Kizayuni. Kwa upande mmoja, mashambulizi ya makombora kwa usahihi mkubwa na kwa malengo mahsusi katika ardhi zilizopokwa yalipelekea hasara kubwa ya watu, mali, miundombinu na hata hadhi ya adui. Kwa upande mwingine, kukabiliana kwa uerevu kwa njia ya ulinzi wa anga dhidi ya mashambulizi ya angani ya adui dhidi ya nchi na watu wa Iran, kulitengeneza kazi ya kipekee kabisa — kazi ambayo haikufurahisha tu kila Muirani Mwislamu na mpenda taifa lake, bali pia ilifurahisha nyoyo za Waislamu na wapenda haki wote duniani, hasa watu wa Afghanistan walio waumini na wenye hisia za kiutu, na iliwatia furaha na fahari katika kina cha nafsi zao.

Katika hali hii, ni lazima na ni wajibu, kwanza kwa moyo wote, kumshukuru Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Amiri Jeshi Mkuu, Ayatollah Imam Khamenei (hafidhahullāh ta‘ālā), na pia vikosi vyote vya kijeshi, kiusalama, kisiasa na kiutawala vya nchi ambavyo vilikuwa waandaaji, waendeshaji na waungaji mkono wa operesheni hii ya kujivunia. Kwa upande mwingine, ni lazima — bila ya shaka — kwa kila Mwislamu mwenye ufahamu kutangaza kwa dhati, kwa uzito na kwa upana uungaji mkono wake kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa kuwa utawala wa kifisadi, wa kivamizi na muua watoto wa Israel ni uvimbe wa saratani ambao kuendelea kwa uhai wake si tu kunaiathiri kanda nzima, bali dunia yote kwa ujumla, hasa katika nyanja za kiusalama, kitamaduni, kijamii na kiuchumi, na sasa unakaribia kuvunjika. Kukabiliana na utawala huu na kujitahidi kuuondoa kabisa katika uso wa dunia, si tu ni jukumu la kidini na kibinadamu, bali ni sharti la awali la kufanikisha usalama wa kweli, maendeleo ya kiutamaduni, ustawi wa kiuchumi na kurejesha heshima kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa hiyo, vita vya taifa la Iran dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni, si tu ni hatua ya kitaifa, bali ni jukumu la kimataifa, Kiislamu na kibinadamu linalofanyika kwa maslahi ya kanda nzima na dunia yote, hasa Ummah mkubwa wa Kiislamu.

Kwa msingi huo; mimi na wenzangu wote wa taifa hili, sambamba na kutoa shukrani na kupongeza uongozi na mihimili yote ya mfumo huu ambao umechukua msimamo huu madhubuti wa kukabiliana na mharibifu wa amani wa maeneo ya dunia — yaani utawala wa kifisadi wa Israel — na ambao hawana shaka yoyote katika kukabiliana na kuukandamiza na kuufuta kabisa juu ya uso wa ardhi, bali wana azma thabiti, tunatangaza kwa nguvu na kwa msimamo thabiti uungaji mkono wetu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama mhimili wa mapambano haya ya kihistoria kati ya Uislamu na ukafiri, tauhidi na uzushi, wanyonge na madhalimu.

اللَّهُمَّ سَلِّمْ، وَاحْفَظْ، وَانْصُرْ جُیُوشَ الْمُسْلِمِینَ مَعَ قَائِدِنَا الإِمَامِ الْخَامِنَه ئی أَیّدهُ‌اللَّهُ تَعَالَی.

Ewe Mwenyezi Mungu! Wape salama, wahifadhi, na waunge mkono majeshi ya Waislamu pamoja na kiongozi wetu, Imam Khamenei — Mola amtie nguvu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha